Mkurugenzi wa NHK Bi. Yuko Asano akisoma hotuba kumkaribisha mgeni rasmi katika sherehe ya uzinguzir wa kurusha matangazo ya NHK kupitia TBC FM. Sherehe hiyo imefanyika katika makao makuu ya TBC Pugu road. Bi. Asano akisisitiza jambo katika hotuba yake. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC Bw. Clement Mshana. Meza kuu. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa ni Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Okada. Mshereheshaji, Mtangazaji nguli wa NHK, Bw. Bakari Msulwa. Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Bw. Clement Mshana Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Okada akisoma hotuba yake kwa lugha ya Kiswahili katika sherehe ya uzinduzi huo. Wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hiyo. Mwenyekiti wa Bodi ya TBC akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Michezo na Utamaduni. Bw. Clement Mshana akitia saini mkataba wa kurusha matangazo ya NHK kupitia TBC FM Wageni waalikwa wakiwemo wasikilizaji wa NHK kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na hata pamoja na nchi za jirani Kenya na Uganda walihudhuria hafla hiyo. Baadhi ya wapenzi wa radio NHK wakifuatilia kwa makini sherehe hiyo. MC Bakari Msulwa. Mjapani bingwa wa kupiga marimba na kuimba nyimbo kwa lugha ya Kigogo.